Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu
kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita
ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale
Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege
Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna
utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao
hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni
ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia
kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu
aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za
kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake,
alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria
wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe
mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu
kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum,
ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni
sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka
chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa
bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya
kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.
Unataka kupata stori kamili? sikiliza AMPLIFAYA ya Clouds FM leo saa
moja usiku, pia kwa Breaking News, habari yoyote ambayo ni habari,
vituko, vichekesho, videos na music na mengine… jiunge kuwa mwanachama
wa millardayo.com kupitia facebook https://www.facebook.com/millardayo
au twitter https://twitter.com/millardayo pia instagram.com/millardayo
ili uwe wa kwanza kutupiwa link kila tukio linapoandikwa.
Wednesday, 31 July 2013
Baada ya Watanzania kukamatwa na dawa za kulevya, hiki ndio kimemkuta Madee akiingia Afrika Kusini
07:37
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment