Timu
ya Ndanda Fc kutoka Mtwara imekuwa timu ya pili kukata tiketi ya
kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya Jumatatu ya March 24 kuibuka
na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Dar mechi iliyochezwa Uwanja wa
Karume 88.5 Dar es Salaam.
Ndanda imepata nafasi hiyo baada ya kuongoza Kundi A la Ligi Daraja
la Kwanza ikiwa na pointi 28 na kufuatiwa na African Lyon yenye pointi
27 na Jumatatu March 24 Lyon ilitoka sare ya bao 1-1 na Green Warriors.
Kwa hatua hiyo Ndanda inakuwa timu ya kwanza kutoka Wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara kucheza Ligi Kuu Bara ambapo awali timu ya Bandari Mtwara
ya Mtwara Mjini ndiyo ilikuwa timu ya mwisho kucheza ligi kuu mwanzoni
mwa miaka ya 2000.
Hizi ni picha za mapokezi hayo yaliyoanzia uwanja wa Ndege wa Mtwara
kisha kuelekea uwanja wa Nangwanda Sijaona na ratiba itakamilika baadaye
kwa kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde Beach.
source; millardayo.com
Friday, 28 March 2014
Namna timu ya Ndanda FC ilivyopokelewa Mtwara Jioni ya leo March 28.
08:43
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment