Saturday, 5 April 2014

Angalia hapa official video ya One campaign – Cocoa na Chocolate

dd
Ile video waliyorekodi wasanii 19 kutoka bara la Africa kwenye kampeni ya kuhamasisha kilimo imetoka.
Angalia jinsi wasanii wengi kutoka nchi za Africa walivyojumuika pamoja kutengeneza video hii wakiwemo A.Y na Diamond.

Tuesday, 1 April 2014

CHEKI VIDEO MPYA YA SHISHI (SHILOLE) BABY CHUNA BUZI

shishi-chuna-buzi-1
Mbali na kuwa ni video mpya lakini ni video ambayo inaingia kwenye headline hasa hapa zilipofanywa video mbili ambazo zote zimetayarishwa na Director mmoja,Chuna Buzi ndiyo jina la wimbo huu ambao mbali na kuwa kwenye wimbo siku chache zilizopita Shilole ali-amplify taarifa za kufungua mgahawa wenye jina hilo.
Audio imefanywa kwa Mazuu pale Mazuu Records na video imefanywa na Nisher ambaye ndiye alie Direct video yake ya wimbo wake uliopita wa Nakomaa na Jiji.
Bonyeza play kusikiliza.

Tazama vipande vya video waliyoenda kufanya wasanii mbalimbali wa Africa akiwemo Diamond na Ay.

777ed01e98d411e3a0f41253bccf28e0_7
Hivi ni vipande vya video ya wimbo ambao umefanywa na wasanii 19 kutoka Africa ambao walikutana South Africa kwa ajili ya kampeni ya Do Agric ambao ni mradi kutoka One Campaign wimbo huo unaitwa  Cocoa na Chocolate,miongoni mwa Madj walienda kushuhudia uzinduzi huo ni pamoja Dj Fetty kutoka Clouds Fm.
Kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuhamasisha kilimo kwa vijana na wasanii wamekutana Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya uzinduzi wa video hiyo ambao unafanyika leo March 31,zaidi ya wasanii 19 kutoka katika nchi mbali mbali Africa wakiwemo Diamond (Tanzania) D’Bhanji na Femi Kuti (Nigeria), Fally Ipupa (DRC) na wengine wengi.
Video hiyo imekamilika na muda wowote kuanzia leo March 31 itaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.

Hivi ni vipande vya video hiyo.

Watu 6 wamefariki kwenye shambulio lingine la kigaidi ndani ya Kenya

eeeee
Watu sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa  na washambulizi waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.
source: millardayo.co

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...