Watu
sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika
shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini
Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko
miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa
miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya
mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa na washambulizi
waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.
source: millardayo.co
Tuesday, 1 April 2014
Watu 6 wamefariki kwenye shambulio lingine la kigaidi ndani ya Kenya
05:08
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment