Saturday, 5 April 2014

Angalia hapa official video ya One campaign – Cocoa na Chocolate

dd
Ile video waliyorekodi wasanii 19 kutoka bara la Africa kwenye kampeni ya kuhamasisha kilimo imetoka.
Angalia jinsi wasanii wengi kutoka nchi za Africa walivyojumuika pamoja kutengeneza video hii wakiwemo A.Y na Diamond.

Tuesday, 1 April 2014

CHEKI VIDEO MPYA YA SHISHI (SHILOLE) BABY CHUNA BUZI

shishi-chuna-buzi-1
Mbali na kuwa ni video mpya lakini ni video ambayo inaingia kwenye headline hasa hapa zilipofanywa video mbili ambazo zote zimetayarishwa na Director mmoja,Chuna Buzi ndiyo jina la wimbo huu ambao mbali na kuwa kwenye wimbo siku chache zilizopita Shilole ali-amplify taarifa za kufungua mgahawa wenye jina hilo.
Audio imefanywa kwa Mazuu pale Mazuu Records na video imefanywa na Nisher ambaye ndiye alie Direct video yake ya wimbo wake uliopita wa Nakomaa na Jiji.
Bonyeza play kusikiliza.

Tazama vipande vya video waliyoenda kufanya wasanii mbalimbali wa Africa akiwemo Diamond na Ay.

777ed01e98d411e3a0f41253bccf28e0_7
Hivi ni vipande vya video ya wimbo ambao umefanywa na wasanii 19 kutoka Africa ambao walikutana South Africa kwa ajili ya kampeni ya Do Agric ambao ni mradi kutoka One Campaign wimbo huo unaitwa  Cocoa na Chocolate,miongoni mwa Madj walienda kushuhudia uzinduzi huo ni pamoja Dj Fetty kutoka Clouds Fm.
Kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuhamasisha kilimo kwa vijana na wasanii wamekutana Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya uzinduzi wa video hiyo ambao unafanyika leo March 31,zaidi ya wasanii 19 kutoka katika nchi mbali mbali Africa wakiwemo Diamond (Tanzania) D’Bhanji na Femi Kuti (Nigeria), Fally Ipupa (DRC) na wengine wengi.
Video hiyo imekamilika na muda wowote kuanzia leo March 31 itaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.

Hivi ni vipande vya video hiyo.

Watu 6 wamefariki kwenye shambulio lingine la kigaidi ndani ya Kenya

eeeee
Watu sita wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleig jijini Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha milipuko katika migahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichopo karibu na zahanati ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa nyingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi watu waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mgahawa huo baada ya mlango wa kutoka nje kufungwa  na washambulizi waliorusha bomu ndani.
Watu hao waliopoteza maisha walikuwa wameenda kununua chakula cha usiku.
source: millardayo.co

Monday, 31 March 2014

Haya ndiyo mauzo ya wimbo wa 2030 wa Roma Mkatoliki kupitia Whatsapp.

ROMAInawezekana kama mitandao ya kijamii ukiitumia vizuri inaweza kukupatia faida kubwa kuna watu kadhaa ambao kupitia mitandao ya kijamii wanendesha maisha yao vizuri miongoni mwao kuna jamaa mmoja anajiita dalali Mkombozi  aliwahi ku-amplify anavyoitumia Instagram kuendesha maisha yake.
whatsapp_APRoma Mkatoliki leo ametoa idadi ya pesa alizowahi kuingiza kupitia wimbo wake wa 2030 ambao alianza kwa kuuza kupitia mtandao wa Whatsapp >>’2030 nilikua nauza kwa shilingi 3,000 kuna artist wanatoa album au mixtape ina nyimbo 20 anauza 5,000 ambao unakuta wanaongea huyo Roma ni nani anatoa wimbo anauza 3,000′
‘Badala ya kusaidiwa na wasanii wenzangu ndiyo wananikandia mi Tanga nina ofisi yangu na napokea album kibao nawauzia tu wana,unakuta watu wanaongea mbona wimbo wenyewe taarifa ya habari halafu anauza 3,000,kwa haraka haraka niliuza kama 1,400,000 kwa kipindi kile cha mwanzo’.
Source 255 Clouds Fm.

Sunday, 30 March 2014

Cheki video ya jinsi MSAGA SUMU alivyopagawisha ndani ya Dar Live .

wemalinex
Kwenye hii video utamuona mkali wa vigodoro anaitwa Msagasumu akiwapagawisha mashabiki wake ndani ya Dar Live ambapo kulifanyika uzinduzi wa movie ya Kigodoro.
Kitu kingine ni pale Wema Sepetu alipoimba verse ya Diamond kwenye wimbo wa Letadutigite akiwa na Linex.
Shilole kahusika pia kwenye hii video bila kuiacha sehemu ambayo Wema alipoamua kuvua pete zote baada ya kupoteza pete moja akiwasalimia mashabiki wake.

Lukas Podolski ni mchezaji wa Arsenal, tazama alichopost kuhusu Tanzania. @Podolski10

Screen Shot 2014-03-29 at 2.33.53 AM
Haijajulikana Podolski alipataje hizi picha ila huyu hapa chini ni Mtanzania alievaa jezi ya staa huyu wa Arsenal ambapo hiki kitendo kimemfanya Podolski kumsifia huyu shabiki kwamba jezi imemtoa freshi na kuitakia kila la kheri Tanzania.
Screen Shot 2014-03-29 at 2.21.16 AM Screen Shot 2014-03-29 at 2.21.24 AM
Hiyo hapo juu ni kwenye instagram ambapo picha hiihii pia aliipeleka kwenye page yake ya twitter kama inavyoonekana hapa chini
Screen Shot 2014-03-29 at 2.37.50 AM 
source: millardayo.com

Hii hapa video ya Amini November – December

amini_november_decemberPicha za behind the scene zilianza kusambaa siku chache zilizopita ambazo zilikua na uhalisia wa hii video itakavyokua,imefanywa na Raymond Kasoga Amini ali-amplify kuwa video hii nayo imefanyika nje kidogo ya jiji la Dar.
Bonyeza play kuitazama.




Friday, 28 March 2014

Picha ya siku ya kwanza Diamond Platnumz anakutana na Wema Sepetu ipo hapa

Screen Shot 2014-03-28 at 4.07.47 AM
Inaaminika katika mapenzi au uhusiano wa kimapenzi uliowahi kuandikwa sana kwenye mitandao na magazeti Tanzania, huu wa mwigizaji Wema Sepetu na Diamond Platnumz umevunja rekodi, mastaa ambao walifikia mpaka kuvalishana pete ya uchumba.
Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.37 AM
Pamoja na yote waliyopitia bado kalamu za Waandishi mbalimbali zilihusika kuwaandika.
Ommy Dimpoz ambae ni rafiki wa Diamond kitambo hata kabla hatawa staa (Ommy) ameshea hii picha inayowaonyesha Wema na Diamond walipokutana kwa mara ya kwanza na kuiambatanisha na hii caption hapa chini.

Screen Shot 2014-03-28 at 1.52.48 AM 
 source: millardayo.com

PENZI LA MR BLUE LAENDELEA KUMTESA NAJ

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambaye huwa anaishi na kufanya Kazi nchini Uingereza Naj amefunguka kuwa Tangu aachane Mr Blue zaidi ya Mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita hajawahi kukutana na Mwanaume na wala hajawahi kumpenda mwanaume yeyote, Naj amefunguka hivi karibuni kabla hajaelekea U.K akaendelea kunitiririkia kuwa alikua na Mr Blue kwa miaka mitano na ikaishia kwa yeye kukimbiwa na Blue akamkana hadharani na kuanzisha mahusiano na mwanadada mwingine hali iliyomhuzunisha na kujutia muda wake, Naj akamalizia kwa kuniuliza Je angeutumia muda huo kwa kupiga kazi si angekua mbali sana? kwa hiyo sasa hivi anacho angalia ni kazi tu kwa kwenda mbele, yuko singoooooooooooooo,

Mr Blue na Naj 
Mr Blue aliachana kwa mbwembwe sana na Naj, kwanza alitokea katika front page ya Gazeti La babkubwa akiwa na Naj na toleo lililofata akatokea katika front page ya Gazeti hilohilo akiwa na mama mtoto wake Wahida kipindi hiyo ana ujauzito wa mtoto wao Sameer



Mr Blue na Wahida 

Mama wa mtoto wa Mr Blue Wahida akiwa na Mtoto wa Sameer, wote wanaishi ndani ya Nyumba Moja
source: tz yakijana.com

Namna timu ya Ndanda FC ilivyopokelewa Mtwara Jioni ya leo March 28.


Image00006Timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara imekuwa timu ya pili kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya Jumatatu ya March 24 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Dar mechi iliyochezwa  Uwanja wa Karume 88.5 Dar es Salaam.
Ndanda imepata nafasi hiyo baada ya kuongoza Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na pointi 28 na kufuatiwa na African Lyon yenye pointi 27 na Jumatatu March 24 Lyon ilitoka sare ya bao 1-1 na Green Warriors.
Kwa hatua hiyo Ndanda inakuwa timu ya kwanza kutoka Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kucheza Ligi Kuu Bara ambapo awali timu ya Bandari Mtwara ya Mtwara Mjini ndiyo ilikuwa timu ya mwisho kucheza ligi kuu mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Hizi ni picha za mapokezi hayo yaliyoanzia uwanja wa Ndege wa Mtwara kisha kuelekea uwanja wa Nangwanda Sijaona na ratiba itakamilika baadaye kwa kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde Beach.
Image00001
Image00004
Image00007
Image00005
Image00011
Image00010
Image00004
Image00003

Image00002
Image00004

source; millardayo.com








Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...