Watu wasiojulikana wamevunja na kuiba nyaraka mbalimbali za jeshi la polisi mkoani Mwanza, huku kamanda wa polisi mkoani humo naibu kamishna Ernest Mangu akihaidi kuwafukuza kazi baadhi ya askari polisi watakaobainika kuhusika katika tukio hilo.
Kamanda Ernest Mangu amewaambia waandishi wa habari jijini Mwanza kwamba watu hao ambao bado hawajafahamika majina yao , usiku wa kuamkia leo wameingia kwenye ghala la kuhifadhia vielelezo na nyaraka la kituo kikuu cha polisi wilaya ya Nyamagana baada ya kuvunja dirisha la ofisi za ukaguzi kanda ya ziwa, na kupora kompyuta ndogo mbili za mkononi ambazo zilikuwa ni vielelezo, nguo za vielelezo vya kesi na kitabu cha kumbukumbu ya matukio na kisha kutokomea kusikojulikana.
Akizungumzia tukio hilo, mkaguzi wa shule kanda ya ziwa Bibi. Florencia Vicent amesema kuwa wezi hao wamevunja madirisha mawili ya ofisi hiyo, ingawa hadi wakati afisa huyo alipokuwa anatoa taarifa hizo walikuwa bado hawajapata uhakika wa kipi kilichoibwa.
Katika hatua nyingine kamanda wa polisi mkoani Mwanza naibu kamishna Ernest Mangu amesema jeshi la polisi mkoani humo limefanikiwa kumkamata mtu anayetuhumiwa kuhusika katika mauaji ya vikongwe katika wilaya za magu na kwamba, ambaye ametajwa kwa jina la Seni Kayende wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment