Wakati mwingine inatia huruma pale anapoonewa bila sababu mtu mpole kabisa na ambae humudu kuzizuia hasira zake hata anapokatwa makusudi uwanjani, mtu ambae hajawahi kushuhudiwa na wengi akifanya ukorofi wowote, mtu ambae sifa yake nyingine kubwa iliyomfanya kupendwa zaidi ni utulivu na anaependa amani.
Sasa imemtokea kwa staa ambae ni raia wa Brazil Ronaldinho wakati Atletico Mineiro walikua wanacheza kwenye Copa Libertadores vs Olimpia ambapo hali ilivurugika kidogo wakati corner kick ilikua inataka kupigwa na mchezaji huyu.
Alishtuka sana pale vitu ambavyo vinaaminika kuwa mawe vilirushwa na baadhi ya mashabiki wa Olympia na kupita karibu na masikio yake ambapo alivichukua na kumuonyesha refa lakini Camera ikaweza kusogezwa na kuviona kwa karibu.
Kwenye hii game Atletico Mineiro ya kina Ronaldinho ilifungwa goli mbili bila……………….. unaweza kutazama hii video hapa chini ujionee mwenyewe ilivyokua.
Friday, 19 July 2013
Uliwahi kufikiria kuna siku utaletewa video kama hii ya jinsi mchezaji mpole kama Ronaldinho alivyotupiwa mawe uwanjani?
12:44
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment