Watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali ya basi mali ya kampuni ya Najimunisa lililokuwa likitokewa jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza baada ya tairi ya mbele ya basi hilo kupasuka na kusababisha kukosa mwelekeo na hatimaye kupinduka katika mji mdogo wa Mbande wilaya ya Kongwa mkoni Dodoma.
Akizungumzia ajali hiyo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda amesema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 491 AUF imetokana na mwendo kasi ambapo mara baada ya tairi kupasuka dereva alishindwa kulimudu na hatimaye kuacha njia na kupinduka huku watu wanne wakipoteza maisha popo hapo huku majeruhi wakikimbizwa katika hosipitali ya rufaa ya Dodoma na hosipitali ya wilaya ya Kongwa. Nao baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wanaelezea namna ilivyotokea
0 comments:
Post a Comment