Juma Mchopanga,
maarufu kama Jay Moe, Mchora Mistari na pia rapper ambaye anaweza sana,
baada ya kukaa katika game kwa miaka mingi sasa, ameamua kuongeza wigo
wa kipaji na sanaa yake kwa kuanza kutengeneza midundo/beats akiwa na
ndoto za kuwa producer mkali katika siku za usoni.
Jay Moe amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huu kutokana na kuwa na uzoefu wa muda mrefu kukaa studios karibu na maproducer wakali - P Funk akiwa namba moja kwenye list, ambapo katika wakati huu wote ameweza kujifunza maujanja mbalimbali ya u-producer.
Rapa huyu amesema kuwa kwa sasa anaendelea kujinoa zaidi kwa njia ya mtandao na kwa njia ya kuwashirikisha maproducer wazoefu na wakongwe kabla ya kuanza kuuza midundo ama kuanza kazi ya production rasmi
0 comments:
Post a Comment