Tuesday, 13 August 2013

EXCLUSIVE: SAKATA LA YANGA VS DILI LA AZAM TV - SERIKALI YAINGILIA KATI - YAWAITA MEZANI

Masaa takribani 24 tangu Raisi wa TFF kuiandikia barua Yanga akiwaambia ameomba maelezo rasmi kutoka kwa kamati ya ligi juu ya mchakato mzima wa namna Azam Tv ilivyoshinda tenda ya kuonyesha mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kuanzia msimu ujao, serikali kupitia wizara ya habari, utamaduni na michezo  imeingilia kati suala hilo.

Habari za kuaminika kutoka chanzo cha habari hii, ni kwamba Serikali kupitia wizara wa Habari, Utamaduni na Michezo imeamua kuingilia kati sakata hilo ambalo limechukua nafasi kubwa katika vyombo hivi karibuni baada ya klabu ya Yanga kushindwa kukabaliana na mchakato mzima wa dili la haki za matangazo ya mechi za ligi kuu msimu ujao kupatiwa Azam TV.

"Serikali imewaita viongozi wa Yanga, Azam Media, TFF na Kamati ya Ligi kwa pamoja siku ya tarehe 14 mwezi huu, saa 5 asubuhi katika ukumbi wa wizara husika ili wafanye mkutano ambao utajaribu kuhakikisha pande zote zinakubaliana kwenye suala hilo kwa munufaa ya mchezo wa soka nchini," kilisema chanzo cha habari hii.

Hatua hii ya serikali inakuja wakati Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuph Manji akiwa ameitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa Yanga juu ya suala hili - mkutano ukiwa umepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.
Credit Shaffihdauda

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...