TUKIO la aibu limetokea Kiwalani jijini Dar Siku ya Idd Pili pale mume wa mtu, Hamad Kipondo (46) alipofariki dunia ndani ya nyumba ya wageni ‘gesti’ akidaiwa kuwa na mke wa mtu ambaye ni mpangaji mwenzake.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu (jina tunalo), Kipondo na mwanamke huyo, Latifa Suleiman (25), ni wakazi wa Kigogo, Dar ambao walifika katika gesti hiyo kwa ajili ya kusaliti ndoa zao.
PICHA KAMILI
Habari kamili zilisema kuwa baada ya mwanaume huyo kuondoka nyumbani, mke aliendelea na shughuli zake kama kawaida huku akiwa hana wasiwasi wowote wa kusalitiwa na mumewe.
SIMU YA KIFO
Ilipotimu saa 8:00 mchana, mke alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimwaambia kuwa mumewe Kipondo amepatwa na matatizo, hivyo anatakiwa kufika haraka Kiwalani.
Mke akiwa hajui kama amepigiwa simu ya kifo, alitafuta usafiri wa haraka wa kuweza kumfikisha Kiwalani ili kujua kile kilichomsibu mumewe.
Njiani alikuwa akitembea huku akiwa na wasiwasi na wakati mwingine aliongea peke yake akiomba Mungu amwepushie balaa mumewe.
MSHTUKO
Mke alipofika eneo la tukio, kwanza alipatwa na mshtuko kwa kuliona gari la polisi aina ya Land Rover 110 ‘difenda’ na watu wakiwa wamejazana.
Moja kwa moja alihisi mumewe alikuwa amekamatwa na polisi, wasiwasi ukaongezeka huku akijiuliza maswali lukuki kwamba kitu gani mumewe atakuwa amekifanya hadi kushikiliwa na askari wale.
VILIO VYAMSHTUA
Kikubwa kilichomshtua mke huyo ni pale alipowaona baadhi ya watu anaowafahamu wakiangua vilio.
Hisia za machozi zikaanza kumvaa bila kujua hasa kilichompata mumewe.
APASULIWA BOMU
Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiangua vilio kwa uchungu na kulitaja jina la mumewe, walipoona mke hajapata picha kamili wakaamua kumpasulia bomu kwa kumwambia kilichojiri.
KILIO
Baada ya kuambiwa kilichotokea, mke huyo akaanza kulia kwa uchungu kuliko mtu mwingine.
Kilio chake kilikuwa na sababu kubwa mbili; kwanza ni kifo cha mumewe, pili usaliti aliofanyiwa.
MBAYA ZAIDI
“Mbaya zaidi marehemu alikuwa na mke wa mpangaji mwenzake na ilikuwa ni Siku ya Idd Pili.
“Kilio kiliongezeka maradufu kwa kuwa alikuwa akimwamini na kushirikiana na mpangaji huyo mwenzake kwa njia moja au nyingine, akijenga uaminifu mkubwa kwamba hawezi kumsaliti,” alisema sosi wetu.
MUME MOCHWARI, MKE WA MTU RUMANDE
Hatimaye polisi waliuchukua mwili wa marehemu Kipondo na kuuingiza kwenye gari kwa ajili ya kuupeleka Hospitali ya Amana kuuhifadhi.
Kwa upande wake Latifa alichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Buguruni, Dar.
CHANZO CHA KIFO
Mpaka habari hii inaandikwa ukweli anao Latifa tu ambaye ndiye anayeweza kusimulia kilichotokea hadi kukatisha uhai wa Kipondo hivyo tunaendelea kufuatilia.
Marehemu Kipondo amezikwa Jumatatu iliyopita katika Makaburi ya Chang’ombe, Temeke, Dar na ameacha mjane na watoto wawili.
0 comments:
Post a Comment