Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini kishule
na kikazi pia. Staa huyo wa Kesho ameshoot video ya wimbo wake mpya
ambao bado haujulikani ni upi mpaka sasa.
Hata hivyo tofauti na video zake za awali, hii mpya amekata kisu kirefu
zaidi kwa kushoot na miongoni mwa gari yenye thamani zaidi duniani,
Ferrari. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa gari hiyo inayotengenezwa na
Waitaliano, imewekewa namba za gari binafsi kwa kuandikwa ‘Platnumz’ na
Wasafi’.
Mafundi wa Afrika Kusini wakihakikisha plate ya Wasafi imekaa vizuri
Inaonekana hii, Diamond Platnumz aka Coca Boy amejiandaa kwenda international zaidi.
Picha: Babutale (Instagram)
0 comments:
Post a Comment