Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt hapo jana alitwaa medali ya dhahabu
kwenye mashindano ya dunia ya mchezo wa riadha yanayoendelea nchini
Urusi .
Bolt alitwaa medali hiyo baada ya kumaliza mbio hizo ndani ya muda wa
sekunde 9.77 ambapo alimaliza mbele ya wakimbiaji toka Marekani na
Jamaica ambao ni Justin Gaitlin na Nestor Carter.
Ubingwa huu ni wa kwanza kwa Bolt tangu mwaka 2009 wakati alipotwaa
ubingwa huo kwa mara yake ya kwanza . Bolt alishindwa kutetea ubingwa
wake kwa mashindano ya mwaka 2011 baada ya kuondolewa kwenye mbio za mia
100 kutokana na kuanza kala ya wenzie ambapo ubingwa huo ulikwenda kwa
Mjamaica Mwenzie Yohan Blake .
Blake kwa bahati mbaya alishindwa kutetea taji lake kwa mashindano ya mwaka huu baada ya kuumia mazoezini .
Wakimbiaji wawili Asafa Powell toka Jamaica na Tyson Gay wameyakosa
mashindano hayo baada ya kugundulika wanatumia dawa zilizopigwa marufuku
wiki chache kabla ya mashindano kuanza .
Monday, 12 August 2013
Usain atwaa medali nyingine .
06:20
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment