Sunday, 18 August 2013

MWAKYEMBE AWATAJA WANAOHISIKA NA KUPITISHA WENYE MADAWA AIRPORT, SOMA HAPA.




Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.




Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni
.



waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.


0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...