Lameck Charles Kanumba anavyoonekana kwa karibu, baada ya kuzungumza mengi
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MDOGO
wake marehemu Steven Charles Kanumba, anayeitwa Lameck Charles Kanumba,
ameibukia jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa kaka yake anamtokea
ndotoni na kuzungumza naye mambo mengi, yanayohusu familia na sanaa ya
Tanzania.
Lameck
aliyasema hayo mapema jana mchana, ikiwa ni miezi mine tangu alipokuja
jijini Dar es Salaam kwenye kumbukumbu ya kaka yake, ambapo pia historia
inafanana kutokana na baba yao kuendelea kula kona na kuacha kuwatunza
watoto wake na kuwatelekeza kwa mama zao.
Charles mdogo wake Kanumba anavyoonekana pichani
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa, Lameck alisema kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es
Salaam, ambapo pia anatumia nafasi hiyo kuhangaikia masuala ya sanaa
ambayo yapo kwenye damu yake.
Marehemu Steven Kanumba.
Alisema
hawajawahi kuonana uso uso kwa Kanumba, kutokana na yeye kuishi mkoani
Mbeya na mama yake, wakati siku anakufa alishindwa kupata nauli ya kuja
kwenye mazishi yake.
“Naendelea
kuumia kutokana na kufariki kwa kaka kabla ya kuzungumza naye uso kwa
uso, lakini pia inashangaza kwakuwa mara kadhaa huwa ananijia ndotoni na
kuzungumza naye hasa mambo yanayohusu familia.
“Baba
hajanihudumia tangu mtoto kama ilivyokuwa kwa kaka Kanumba, hivyo bado
naona nina mengi ya kufanya kwa ajili ya kumuenzi marehemu aliyeifanyia
mambo mema Tanzania kwa kupitia sanaa,” alisema.
Chanzo na uswazi
0 comments:
Post a Comment